Tanzania regional map
Imeundwa kwa sherehe kote Tanzania

Panga, alika na karibisha kila mgeni—kwa mpangilio mzuri.

Kwa hafla yako mwenyewe au hafla za wateja wako—simamia mialiko, RSVP, wageni na mapokezi kutoka workspace moja.

Anza kupanga bila malipo.

Kiswahili na KiingerezaLink rahisi kwa wageniUkaguzi wa haraka kwa simu

ANZA NA TUKIO LAKO

Unapanga tukio gani?

Lipe jina. Tutahifadhi ulipofikia unapofungua akaunti.

  1. 1Taja tukio
  2. 2Fungua akaunti
  3. 3Kamilisha maelezo

Mwanzo wa tukio lako utabaki kwenye kifaa hiki kwa siku saba.

Kwa kuendelea unakubali Masharti ya Huduma na Taarifa ya Faragha.

Dashibodi ya Waalikwa, ikionyesha idadi ya matukio, yanayohitaji uangalizi, na jedwali la matukio yajayo.

Imeundwa kwa namna unavyopanga hafla.

Workspace ile ile, iwe ni sherehe yako mwenyewe au mteja wako wa ishirini mwaka huu.

Hafla yako mwenyewe

Harusi, send-off, mahafali au birthday—wageni wako sehemu moja badala ya kutawanyika kwenye spreadsheet na ujumbe.

  • Pakia orodha ya wageni uliyo nayo tayari
  • Mwaliko mmoja kwa kila mgeni, na viti vyake
  • Jua nani anakuja kabla ya siku yenyewe
Ona mialiko inavyofanya kazi

Waandaaji wa hafla

Simamia hafla za wateja kadhaa kutoka workspace moja, kila moja na orodha yake ya wageni, mialiko na timu.

  • Hafla za kila mteja kwenye kalenda moja
  • Wafanyakazi wa langoni wanaona hafla yao tu
  • Ripoti kwa kila hafla ikiisha
Ona kalenda

Kamati na timu

Gawanyeni kazi za mialiko, majibu, michango na mapokezi mlangoni, kwa majukumu yanayoamua nani anafanya nini.

  • Mwenyekiti, katibu, mtunza hazina, wajumbe
  • Ahadi, malipo na matumizi kwa TZS
  • Rekodi hufutwa kwa sababu, hazibadilishwi
Ona michango

Uwe yeyote kati ya hao, huanza vivyo hivyo.Lipe tukio lako jina

Siku ya tukio iliyorahisishwa

Kutoka orodha ya wageni hadi langoni, na hesabu zake.

Kila skrini hapa chini ni bidhaa halisi, si mchoro. Hii ndiyo safari nzima ya mwandaaji, kwa mpangilio.

Panga

Kila kipindi cha kila siku, kwenye kalenda moja.

Harusi mara chache huwa tukio moja. Weka mapokezi, ndoa na sherehe kama vipindi tofauti, kisha uviangalie kwa siku, wiki, mwezi au mwaka.

  • Matukio ya siku nyingi, hata kipindi kinachovuka usiku wa manane
  • Chagua mkoa, wilaya na kata—vimeundwa kwa Tanzania
  • Rasimu, hai, limekamilika na limeghairiwa, kila moja kwa rangi yake
Kalenda ya Waalikwa kwa mwezi, ikiwa na matukio na vipindi vyenye rangi kwa kila wiki.

Alika

Mwaliko wa kila mgeni, kwa WhatsApp au SMS.

Tengeneza sanaa kwa kila mgeni, ikiwa na jina lake na kile mwaliko unachoruhusu. Unatuma kila mmoja mwenyewe, kutoka WhatsApp yako, ili ufike kutoka namba ambayo wageni wako wanaijua.

  • Msimbo unaosomeka kwenye kila kadi, wa mgeni huyo pekee
  • Familia, wanandoa au mmoja—pamoja na idadi ya viti
  • Hayupo WhatsApp? Mtumie link kwa SMS moja kwa moja kutoka Waalikwa
Skrini ya mialiko, ikionyesha sanaa ya mwaliko kwa kila mgeni na vitufe vya kupakua na WhatsApp.
Mwaliko kama mgeni anavyouona kwenye simu yake, ukiwa na sanaa na vitufe vya kukubali au kukataa.

Unatuma

Umealikwa. Fungua mwaliko wako: waalikwa.app/i/9FFE8U

Anabonyeza link

Thibitisha

Nani anakuja, bila spreadsheet hata moja.

Majibu huingia yanapofika. Mgeni akipiga simu badala ya kubonyeza, wafanyakazi wako wanamwandikia na yeye anapata uthibitisho kwa SMS.

  • Watakaohudhuria, waliokataa na ambao hawajajibu, kwa mtazamo mmoja
  • Wafanyakazi wanaweza kuandika jibu lililotolewa kwa simu
  • Tafuta kwa jina, simu au msimbo wa mwaliko
Skrini ya majibu, ikiwa na kadi za kuchuja watakaohudhuria, waliokataa na wanaosubiri, na orodha ya majibu.

Karibisha

Langoni hufanya kazi kwa simu, na huhesabu viti.

Changanua msimbo au tafuta jina. Familia ya watu sita inaweza kufika kwa makundi mawili na viti bado vikahesabika sawa—na hakuna anayeingizwa mara mbili.

  • Changanua msimbo kwa kamera, au mtafute mgeni mwenyewe
  • Ingiza baadhi ya viti sasa na vingine watakapofika wenzao
  • Kila kuingiza kunathibitishwa mara moja na hakuhesabiwi mara mbili
Skrini ya kuingiza langoni kwenye simu, ikionyesha viti vilivyobaki vya mgeni na kitufe cha kumwingiza.

Toa hesabu

Michango, na hesabu za kuionyesha.

Ahadi zilizotolewa kwenye kikao cha kamati, malipo yanapoingia, na pesa ilipoenda—pamoja na orodha ya kushukuru ya kila aliyeingia langoni kweli.

  • Ahadi, malipo na matumizi kwa TZS, kwa kila mchangiaji
  • Rekodi hufutwa kwa sababu, haibadilishwi kimyakimya
  • Mahudhurio, saa za kufika, na wa kushukuru baadaye
Daftari la michango, likionyesha jumla ya ahadi, zilizokusanywa na zilizotumika, na chati ya matumizi kwa aina.
Ripoti ya tukio, ikionyesha mahudhurio, chati ya wageni walipofika, na orodha ya kushukuru.

Na ripoti baadaye

Uzoefu wa wageni wako, umeandaliwa kwa umakini.

Rahisi kwa sherehe ndogo na imara kwa timu nzima—bila kuwalazimisha wageni kufungua akaunti.

Anza na tukio lako lijalo

Anza na tukio lako lijalo

Lipe jina na uchague tarehe. Kila kitu hapo juu kinakusubiri upande wa pili.

Kiswahili na KiingerezaLink rahisi kwa wageniUkaguzi wa haraka kwa simu

ANZA NA TUKIO LAKO

Unapanga tukio gani?

Lipe jina. Tutahifadhi ulipofikia unapofungua akaunti.

  1. 1Taja tukio
  2. 2Fungua akaunti
  3. 3Kamilisha maelezo

Mwanzo wa tukio lako utabaki kwenye kifaa hiki kwa siku saba.

Kwa kuendelea unakubali Masharti ya Huduma na Taarifa ya Faragha.